Shemeji Lumbe
Daudi Kabaka
3:45Msichana wa sura nzuri Kitu gani kinakufanya usiolewe Elimu unayo ya kutosha Hata ng’ambo ukaenda ukarudi Msichana wa urembo kama wewe Uonyeshe mapenzi kwa vijana Ukionyesha majivuno kwa vijana Utazeeka ukiwa nyumbani kwenu Ooh baby, miaka yaenda mbio sana Na sura yako nayo ikichuchuka Ooh baby, miaka yaenda mbio sana Na sura yako nayo ikichuchuka Pengine tabia zako ndizo mbaya Awali kweli dada ulijivuna Kwanza mimi nilitaka nikuoe Ukaringa ati sina masomo Ooh baby, ona watoto wa nyuma yako Wameolewa wamekuwacha ukihangaika Ooh baby, ona watoto wa nyuma yako Wameolewa wamekuwacha ukihangaika Msichana wa sura nzuri Kitu gani kinakufanya usiolewe Elimu unayo ya kutosha Hata ng’ambo ukaenda ukarudi