Si Uko Tayari

Si Uko Tayari

Diamond Platnumz

Альбом: Kamwambie
Длительность: 3:31
Год: 2013
Скачать MP3

Текст песни

Mmh mmh mmh
Mmh mmh hahieya
Mmh mmh mmh, mmh

Hadithi za mapenzi, zina safari safari safari za mbali
Visa na mambo mengi, vinatesa unajua ila mpenzi usijali
Na sumu ya mapenzi, inatesa moyo mchana, usiku silali
Sukari ya mapenzi, ishaganda moyoni zaidi ya tamu ya asali

Tazama uzuri wako, penzi langu usije shusha thamani
Thamani ya penzi lako, nitalitunza moyoni na kesho peponi
Tazama uzuri wako, penzi langu usije nishusha thamani
Thamani ya penzi lako, nitalilinda moyoni na kesho peponi
Dunia na mapenzi, vinatesa unajua sema mpenzi tafadhali
Usiku silali, ooh lalalaah

Nauliza uko tayari
Nikupeleke nyumbani, japo sina pesa na nyumba gari
Usijali
Nauliza uko tayari
Nikupeleke nyumbani, japo sina pesa na nyumba gari
Usijali

Ona
Yupo niliompenda, kwa utenzi na nyimbo na zeze nilimwimbia
Akaniacha akaenda, na maradhi ya kupenda moyoni nikaugulia
Yupo niliompenda, kwa utenzi na nyimbo na zeze nilimwimbia
Akaniacha akaenda, na maradhi ya kupenda moyoni nikaugulia

Masikini penzi langu, sina pesa, mali na gari za kuringishia
Chondechonde roho yangu, na simanzi ya mapenzi moyoni nisije kulia
Masikini penzi langu, sina pesa, gari na mali za kuringishia
Chondechonde roho yangu, na simanzi ya mapenzi moyoni nisije kulia
Dunia ya mapenzi, vinatesa unajua sema mpenzi tafadhali
Maumivu ya mapenzi, yanatesa moyo mchana usiku silali

Nauliza uko tayari
Nikupeleke nyumbani, japo sina pesa na nyumba gari
Usijali
Nauliza uko tayari
Nikupeleke nyumbani, japo sina pesa na nyumba gari
Usijali

Oh oh eyah, mmh mmh
Oh oh eyah, uko tayari
Oh oh eyah
Usijali

Oh oh eyah, mmh mmh
Oh oh eyah, uko tayari
Oh oh eyah
Usijali