Funguo (Feat. Martha Mwaipaja)

Funguo (Feat. Martha Mwaipaja)

Florence Andenyi

Альбом: Funguo
Длительность: 5:55
Год: 2023
Скачать MP3

Текст песни

Yesu nipe funguo,baba nipe funguo,
Yesu nipe funguo kwa huduma yangu,
Yesu nipe funguo,baba nipe funguo,
naomba unipe funguo kwa maisha yangu

Nipe funguo baba ,nipe funguo yahweh,
Oh naomba funguo,

Naamka asubuhi naenda tafuta riziki,
Naondoka naenda tafuta riziki,
Ili niwalishe ndugu na jamaa zangu,
Nikifika milango imefungwa,
Nikifika milango imefungwa,
Oh naomba funguo,
Yesu nipe funguo,

Nipe funguo,(nipe funguo)
Nipe funguo,(Mwenyewe nimeshindwa Bwana)
Naomba nipe funguo kwa maisha yangu (nipe funguo)
(Nataka kwenda mbali) nipe funguo,
(Nimefika Mwisho)nipe funguo
(Nipe kushinda haya Bwana) naomba nipe funguo kwa maisha yangu (nipe funguo Bwana)

Nimetoka mbali mimi,
Nimejitahidi sana,mimi
Nimejitahidi sana kuyashinda haya magumu
Nimekimbia sana mimi,
Nimetembea sana mimi baba,
Imefika wakati sasa nimechoka,
Miguu yangu imelegea nimekosa nguvu,
Maana nilifikiri hapa kutakuwa mwisho wangu,
Kumbe bado safari ninayo,
Kumbe bado natakiwa kuendelea,
Nami baba nipe funguo,
Ili nifike pale ,nipe funguo,
Milango ya pale yote imefungwa,
Nipe funguo,baba

Nipe funguo,(eh naomba)
Nipe funguo,(Yesu nipe funguo)
Naomba nipe funguo kwa maisha yangu
(Usiniache niteseke) nipe funguo,
(Baba nipe funguo) nipe funguo
(Ooh nipe funguo baba) naomba nipe funguo kwa maisha yangu (Oh Eh)

Hela ya kodi nimelemewa nyumba nimefungiwa,
Marafiki wananicheka,bwanaa,
Nimekosa tumaini,nimekosa msaada,
Msaada wangu watoka wapi eh baba,
Kupitia kwa moto nimepitia mie,
Kama ni gharama,nimelipa mie,
Kupitia kwa moto nimepitia mie,
Oh kama ni gharama nimelipa mie,
Oh Yesu nipe funguo,baba nipe funguo,
Baba nipe funguo Yahweh

Nipe funguo,(nataka kushinda bwana)
Nipe funguo,(Sitaki Nipotea)
Naomba nipe funguo (eeh baba)kwa maisha yangu
(Naomba nisikie Bwana) nipe funguo,
(Mimi Ninakusubiri) nipe funguo
(Baba nitasubiri) naomba nipe funguo kwa maisha yangu (Oh Eh)

Mmh,wewe ni tabibu ganga jeraha zangu,
Moyo unalia mimi nakusubiri,
Hatua zangu ni fupi siwezi kwenda mwenyewe,
Baba siwezi bila wewe oh,
Baba siwezi bila wewe oh,
Ukinishika mkono wako,
Nitaenda mwenyewe,
Ukinishika mkono wako nitaenda vizuri

Nipe funguo,(eh naomba)
Nipe funguo,(Yesu nipe funguo)
Naomba nipe funguo kwa maisha yangu
(Usiniache niteseke) nipe funguo,
(Baba nipe funguo) nipe funguo
(Ooh nipe funguo baba) naomba nipe funguo kwa maisha yangu (Oh Eh)