Champion (Feat. Nay Wamitego)

Champion (Feat. Nay Wamitego)

Kontawa

Альбом: Champion
Длительность: 3:27
Год: 2022
Скачать MP3

Текст песни

(Jam on the beats)

Eh! Oya mitaa niliotoka police wanauza gongo
Hata uwe mkweli huwezi ishi bila uongo
Mlo mmoja na bado tulibeba nondo
Na maisha yakasonga tu

Eh! Ili sabuni zisiishe tulinyoa madongo
Tulakala maharage hadi tukawa wachezaji wa ndondo
Oh si' tumetokea Bongo na maisha ya nasonga tu, oh yeh

Nishazika wanagu nilowapenda
Ukija mtaani kwangu kutwa defender
Kukimbizana January mpaka December
Aah, eh-eh!

Chumba kimoja wanalala dada na kaka
Watu hawatupi msosi hata ukichacha
Baba jambazi, mtoto anajiuza mataani
Mama mchawi nyumbani atabaki nani?

Ah-yeah, I'm the winner
I'm the champion
Ah-yeah, I'm the winner
I'm the champion

Eh!
Tumeishi na watu wanaoamini kwenye mpango wa Mungu kuna mkono wa mtu
Tumeishi na watu wanaoamini sikukuu ndio siku ya kuchinja kuku, oya we (oya we)
Tumeishi na watu wanaotembea na umeme lakini bado nyumbani walikosa luku (walikosa luku)
Eh! Tukaishi na watu ambao wanaoamini kwamba bahati-Bahati zote alipangiwa Bukuku

Hapo mwanzoni waliamini hatutopata mafanikio
Waliotufagilia wakauza mafagio
Eh! Mtaani kwetu sio
Mtu aliotoboa sana alitoboa sikio

Chumba kimoja wanalala dada na kaka
Watu hawatupi msosi hata ukichacha
Baba jambazi, mtoto anajiuza mataani
Mama mchawi nyumbani atabaki nani?

Ah-yeah, I'm the winner
I'm the champion
Ah-yeah, I'm the winner
I'm the champion (champion, champion)

Wimbo unanikumbusha mbali kipindi naitwa Ima'
Dharau, kejeli, manyanyaso ka' yatima
Na ivyo ndo vimenikomaza mpaka leo nimesimama
Ah! I thank God kwa hii power na heshima

Ni'shatembea kwa miguu toka Manzese mpaka Temeke
Kuomba nafasi ya kuimba na bado na iyo sipati
Dharau zao na manyanyaso mli'fanya tamaa n'sikate (dah!)
Pumzi inakata, koo linakauka

Na bahati mbaya hata mdomoni sina mate!
N'kapiga moyo konde n'kamuomba Mungu niongoze
Na nikaweka nia kwamba mziki utanilisha
Mziki utanivisha, mziki utanitajirisha

Maisha ya zamani hayafanani na ya sasa
Ni'sha sota sana acha tu nile bata
Ma-deal mengi sikuizi, na sign angani
Naitwa Raisi wa kitaa, napendwa mtaani

Ah-yeah, I'm the winner
I'm the champion (champion, champion, champion)
Ah-yeah, I'm the winner
I'm the champion (champion, champion, championi)

Mi' nachekaga tu
Yeah!
(Mafiaa)