Notice: file_put_contents(): Write of 642 bytes failed with errno=28 No space left on device in /www/wwwroot/muzbon.net/system/url_helper.php on line 265
Martha Mwaipaja - Naiona Kesho | Скачать MP3 бесплатно
Naiona Kesho

Naiona Kesho

Martha Mwaipaja

Альбом: Naiona Kesho
Длительность: 9:14
Год: 2016
Скачать MP3

Текст песни

Naiona kesho, kesho iliyopangwa na Baba
Naiona kesho, kesho iliyopangwa na Mungu
Naiona kesho mimi, kesho iliyopangwa na Baba
Kesho ya heshima ah, iliyopangwa na Baba

Kesho ya neema ah, iliyopangwa na Baba
Kesho yenye utukufu, iliyopangwa na Baba
Kesho ya kuinuliwa ah, iliyopangwa na Baba
Kesho ya ushindi, iliyopangwa na Mungu
Kesho yenye nguvu, iliyopangwa na Baba

Sitaki kuitazama leo yangu, mwenzenu
Sitaki kuitazama leo yangu, mwenzenu
Leo yangu ni shida ah, mwenzenu
Leo yangu ni taabu, mwenzenu
Leo machozi yanitoka ah, mwenzenu
Leo nimekataliwa ah, mwenzenu
Leo nimefukuzwa mapema, mwenzenu
Leo wote waniacha ah, mwenzenu
Leo machozi ni mengi, mwenzenu

Sitaki kuitazama leo yangu, kamwe
Sitaki kuitazama leo yangu, mimi
Leo yangu ninalia, mwenzenu
Leo ninateseka ah, mwenzenu
Leo mateso ni mengi, mwenzenu
Naiona kesho yangu, mwenzenu
Naiona kesho yangu, mwenzenu

Japo vita yangu ni kubwa, mwenzenu
Maadui wangu ni wengi, mwenzenu
Japo mateso yangu ni magumu, mwenzenu
Kuna neno amesema nami, mwenzenu
Atapigana ah, amesema
Atafanya mlango oh, amesema
Atanifanyia wepesi, amesema

Japo vita yangu kubwa, mwenzenu
Japo adui ni wengi, mwenzenu
Japo njia siioni, mwenzenu
Atapigana mwenyewe, amesema
Atafanya wepesi, amesema
Atanifanyia wepesi Bwana, amesema
Atanichunga salama, amesema
Atafanya mlango oh, amesema
Atapigana na adui ah, amesema

Kasema niione kesho aliyoniwekea
Kasema niione kesho aliyoniwekea
Kuna majira yalifika nikajua Mungu
Kuna majira yalifika nikamwelewa
Majira yale yalikuwa magumu
Majira yale yalikuwa ngumu
Kwa macho yangu nikaona akitenda

Kwa macho yangu nikaona akitenda
Akasema, "Mwanangu, nakupenda"
Akasema, "Mwanangu, nakupenda"
Usiitazame leo yako, mwanangu
Usiitazame leo yako, mwanangu
Mbona mimi ni Mungu, nikupendaye
Mbona mimi ni Mungu, nikupendaye

Ni kweli kwa macho ya nyama, mimi nimechoka
Wengi wanitazamapo, kweli nimeshindwa
Wengi wanionavyo, kweli nimeshindwa
Kweli kwa mbio za mimi nimechoka
Kweli kwa mwendo wangu nimeshindwa
Kwa macho ya nyama nimechoka
Kwa macho ya watu nimeshindwa
Lakini hakuna hata mmoja
Anayejua patano langu na Mungu, oh

Lakini hakuna hata mmoja, ah
Anayejua nimepatana nini
Tumepatana na Baba, hataniacha
Hata nikisukwa, sukwa sitamuacha
Hata nikilia, nisimwache
Hata nikiteseka ah, nisimwache

Tumepatana na Baba
Nimepatana na Baba
Nimepatana na Baba
Nimepatana na Baba
Naiona kesho yangu iliyonjema, ah
Naiona kesho iliyonjema, ah
Mwenzenu, naiona kesho

Naiona kesho, kesho (kesho) iliyopangwa na Baba (kesho ya heshima)
Naiona kesho, kesho, (ah) iliyopangwa na Mungu (kesho ya neema)
Naiona kesho, kesho, iliyopangwa na Baba (kesho ya kufanikiwa)
Kesho ya heshima ah, (kesho, kesho, kesho ya utukufu)
Iliyopangwa na Baba
Kesho ya ushindi (kesho ya heshima yangu na mimi)
Iliyopangwa na Mungu
Kesho ya heshima, iliyopangwa na Baba (oh, kesho)

Naiona kesho, kesho, iliyopangwa na Baba (Baba, kesho, kesho, kesho ya neema)
Naiona kesho, kesho, iliyopangwa na Mungu (kesho ya heshima)
Naiona kesho, kesho (kesho, ya wote kumjua Mungu wangu)
Iliyopangwa na Baba
Kesho ya heshima, ah (kesho, kesho), iliyopangwa na Baba
Kesho ya ushindi, iliyopangwa na Mungu (kesho ya heshima, kesho, kesho, ah)
Kesho ya heshima ah, (kesho ya utukufu wangu), iliyopangwa na Baba
Kesho, kesho, kesho, ah