Kipi Sijasikia (Feat. Diamond Platnumz)

Kipi Sijasikia (Feat. Diamond Platnumz)

Professor Jay

Альбом: Kipi Sijasikia
Длительность: 4:06
Год: 2020
Скачать MP3

Текст песни

Niliacha kazi kufanya mziki
Wakatabiri ntalosti
Wengine wakashawishi tuloge kuondoa mikosi
Nakomaa na mziki ingawa jua la utosi
Naamini wote tunapita na kamwe maiti haijioshi

Jina langu lisha tumika sana kutajilisha watu
Nyota ndogo asha sema kuna watu na viatu
Bunduki haiui watu ila watu ndo wanau watu
Dunia kama jalala tazama kwa jicho la tatu

Ni saa mbaya
Watu wana husda na roho mbaya
Tunawaita watakatifu kumbe ni mavimpire
Yalisemwa mengi

Demu wangu alipo toroka
Ni fundisho tosha
Na changamoto kwa mwana choka
Nimepitia mengi mitihani ya kila namna
Ndo maana sishangai wakiniita mbeba lawama

Washikaji wengine feki kwenye shida hawakujui
Wanazani kila jogoo akiwika niasubuhi.
Liziki hamwezi ziba
Labda mtaichelewesha tuu
Mnakesha mnanishusha mwenyezi ananipaisha

Kote mliko bana
Kidume ndo natusua
Mnanijua nakamua
Roho za wanga zinaungua.

Unaehukumu ni wewe
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita mie
Nami nishike mkono nishinde

Unaehukumu ni wewe
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita mie
Mwanachonga daima nishindwe

Walisha zusha nimekua
Eti nimepata ajari
Washindwe na walegee
Mweyezi niepushe mbali

Wakasema nina ukimwi
Kwakua nilikonda ghafla
Wanataka kunizika mzima kabla sijafa

Walo sema nina ngoma
Wengine tusha fukia
Wanaomba nife leo
Naamini watatangulia

Mama pumzika pema
Daima tunakulilia
Na bado wanachonga sana
But men the king is here

Daima mtaji wangu
Ni nguvu zangu mwenyewe
Simwamini mtu kamwe
Najiamini mi mwenyewe

Hata nikinwya maji
Wanadai nakunywa pombe
Mi sijali I knock them all
Wanalizombe

Bado tunapigana
Kibarua kisiote nyasi
Daima sito wadhuru
Wale wote walio niasi

Nikikaa kimya
Msizani sijasikia
Sio bahati
Sio ngekewa
Ni sauti ilio barikiwa

Unaehukumu ni wewe
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita mie
Nami nishike mkono nishinde

Unaehukumu ni wewe
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita mie
Wanachonga daima nishindwe

Mungu walaze pema
Waliisema kajiua
Ingawa wote tunapita
Naamini maisha ni hatua

Maneno ya watu sumu
Yanaponya na yanaua
Pliz nipe ujasiri
Mpaka siku ukinchukua

Wape nguvu wale wote walio kata tamaa
Maneno yanaleta hila na mizozo kwenye mitaa.
Wanaesabu mabaya tuu

Na mema hawayaoni
Wanakuchekea machoni
Wanakuloga moyoni
Wanacheka chinichini

Wakati una msiba
Wakwanza kukutangaza
Kwa watu ukiwa na shida.
Wantamani wapangue
Kila mora alicho panga
Wanatangaza amani
Huku wameshika mapanga

Unaehukumu ni wewe
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita mie
Nami nishike mkono nishinde

Unaehukumu ni wewe
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita mie
Wanachonga daima nishindwe

Thai...
Mi maneno nsha zoea (aaaah)
Ndo maana sijali wanapo ongea (aaah eeeeh)
Wanasema maneno mengi mengi mengiiii... Ehieh