Kanisa La Mungu
The Saints Ministers
5:47Chorus Sasa ni zamu yangu huu ni wakati wangu, ule mwaka wa baraka ulioniahidia, pokea Sala zangu uzijibu baba ikiwa ziko ndani ya mapenzi yako, pokea sifa zangu na shukrani baba kwa kuwa hujawahi kuniangusha Stanza 1 Nilipokubali kukufuata nikatengwa mbali na watu (ukasema wewe ni Mungu kwako Niko salama) watesi wangu walipojipanga kunimaliza, ..... Pamoja na changamoto nitasimama na wewe Yesu (umesema wewe ni Mungu kwako niko salama) .. (Najua sitaanguka nitasimama milele hata tufani zikivuma) nitadumu kuwa nawe. Chorus Stanza 2 Kunawakati Imani yangu inapitishwa motoni, saa nyingine kuanguka, nimejifunza kusimama tena, nimejifunza kuvumilia nikikumbuka ahadi yako hofu inapungua. Kuna wakati ninayumbishwa kibinadamu, machozi kutiririka kwa maumivu kunawakati nilisahau kusimama juu ya mwamba ninakuomba baba yangu nipe moyo mkuu.