Jivunie Chako
Zabron Singers
5:29Verse 1 Naogopa nikiwambia watu sijui wataniona vipi! Naogopa kuyasema yote acha tu ninyamaze kimya ( hey hey hey) Naogopa kuwaambia watu wanaanza kuniseng`enya Nina maswali Mengi Miguuni pako Kwa nini Mungu umekuwa kama vile huoni Pesa sina lakini umeacha niuguee Namtegemea lakini umemwacha aondoke Kwa nini Mungu umenyamaza aaaaa Chorus Mawimbi ni makali ,upepo ni mkali naa mlima ni mkali umenyamaza! Maumivu na makali na vita ni vikali nimevumumilia nimeshindwa Sema kitu Verse 2 Ona kwa yule ulitenda juzi na leo tena, kuna ugumu gani kwangu Baba sema basi Mimi binadamu nakosa majibu sema Baba Nakuamini sana Baba yangu usiniache Kuna shida gani! Imekuaje! hata usiseme kama ni kosa naomba unisamehe Turekebishe naomba unisamehe, nitateta nawe sitakata tamaa wakuamua yangu bado ni wewe Na kuamini Mungu Bado ni wewe Naogopa huko kimya kuna nini Mungu sema neno usikae Kimya nisije kufuru Mungu Kama siku zangu za kuishi duniani bado zipo oo naomba sasa Baba umalize umalizane na shida zanguu Mambo mengii nimeomba kwako umejibu hili hujajibu Mungu wangu bado nasubiri kwako Jibu basi watu wakuone wewe watu wakuone Baba bado nasubiri kwaako.