Sometimes (Feat. Lydia Marley)
Rapcha
3:04Takataka Takata Takataka Takata Takataka (What is Dead may never die.. what is Dead may ne..?) Imetakata Takataka Imekua Dhahabu yang'aa Mshua kutumia tu kondomu yeye alikataa clivyopewa story kuna mimba yangu alikataa Ikabidi mama ndo anipambae japo mwanzo alipoulizwa home ka' anamimba ‘ye alikataa Siku zikamove mara miezi ikajikataa Shule walipojua kuwa ana mimba tu wakamkataa Mwisho wa siku mama ndo akajifungua Maana hakupokea ushauri wa kutoa mimba ye alikataa cdo ado kabla ya kutembea nikaanza kutambaa Mama hakutoa macho yake kwangu kila saa ckipata dili za chapaa aliomba ndugu zake waangalie mtoto ye atoke wote wakakataa Kwa sababu zisizonihusu Majirani kuruhusu ncheze na watoto wao tu walikataa Mvua zikanyesha zikakata nikakua Nikagundua kuwa mshua hakuzingua Ona Takataka leo imetakata Takataka sasa imetakata Takataka Imetakata Takataka Imekua Dhahabu yang'aa Nikaenda shule mwalimu wa hesabu akanikataa Group discussion wale smart wananikataa Nkaanza kujifunza kutongoza sio shule wala mtaa kila binti nnaemtaka ananikataa Kuna ambao kuongea na mimi tu wakakataa Wengine wakaongea ila kunipa namba wakakataa Wengine walinipa kwenye kukutana wakakataa Wengine ndo baada ya kuonana wakanikataa Nkitafuta nafasi ya kushine watu wananikataa Nkiwa lowkey ninaboa wananikataa Vyeti nimetembeza ka' kahawa maofisini Mpaka nguo zangu wamekariri bado wamenikataa Watu wananiambia kuwa kujiriajiri ndo inafaa Nikijiajiri naona kama watu wananikataa Jua linaibuka linazama juu natazama Haya maisha Mungu tu pekee ndo hajanikataa Ona Takataka leo imetakata Takataka sasa imetakata Takataka Imetakata Takataka Imekua Dhahabu yang'aa Kama hukuelewa ule mstari wa mwisho kwenye verse ya kwanza skia ccha niiweke very clear Mshua alizingua tu kwa kile alichofanya pale ambapo ile story ya mimba yangu ilimfikia Mama nae naona hakuwa proud kunibeba muda ule na ndo maana kwa wazazi alikana akaninificha cll my life cll my life cll my life Nitatoka jasho nipende sipendi cll my life Posa hazina idadi nimetuma karibia niimalize Dar Leo wazazi watakubali binti atakataa Ntapoenda kesho binti atakubali wazazi watakataa Kama wote watakubali dini zinakataa Nimeamua kujipenda mimi kwanza Kwa kufanya hivyo siumizwi na yeyote anaenikataa Dunia inazidi kuzunguka natusua Nagundua nahitaji kusamehe walionikataa Ona Takataka leo imetakata Takataka sasa imetakata Takataka Imetakata Takataka Imekua Dhahabu yang'aa Takata Takata (What is Dead may never die.. what is dead may ne..??) Imetakata Takataka Imetakata Takataka Imekua Dhahabu yang'aa