Nitumie Lugha Gani

Nitumie Lugha Gani

Reuben Kigame

Альбом: Usifadhaike
Длительность: 3:52
Год: 2016
Скачать MP3

Текст песни

Nitumie lugha gani
Kutangaza ukuu wako
Eh, Mungu wangu
Ufananishwi
Nitumie sauti gani
Kuimba nyimbo zako
Umetukuka, una mamlaka yote

Ningekuwa na ndimi elfu moja
Ningetangaza jina lako dunia nzima
Ningekuwa na uwezo mkubwa sana
Ningepamba dunia mzima kwa jina lako
Eh, Bwana

Elimu ya mwana damu
Ndimi za malaika
Hazitoshi kusimulia
Hekima, fahamu yako
Uweza na upedo wako
Eh, Bwana, umetukuka sana

Ningekuwa na ndimi elfu moja
Ningetangaza jina lako dunia nzima
Ningekuwa na uwezo mkubwa sana
Ningepamba dunia mzima kwa jina lako
Eh, Bwana

Nyota, ngurumo, bahari umeumba
Ndege na wanyama wa kutegemea
Samaki wadudu, majani vyote vyako
Sisi wana wako, tuseme nini?

Ningekuwa na ndimi elfu moja
Ningetangaza jina lako dunia nzima
Ningekuwa na uwezo mkubwa sana
Ningepamba dunia mzima kwa jina lako
Eh, Bwana... (Eh, Bwana...)