Wapi
Joel Lwaga
3:35Zamani Sikueleweka na wengi Hasa ndugu na rafiki wa karibu Utani walidhania ni utani nilipowaeleza Yesu ndiye Jibu Wengine wakanisanifu Kwa Maswali ya kejeli na dharau Kwamba Kama Yesu ndiye Jibu Mbona maisha yangu yamejaa maswali Ni kweli kwa wakati huo huenda walikuwa sahihi Maana hali niliyokuwa nayo isingeweza kabisa kushawishi Wengi walidhani napoteza muda Wengi walidhani nimechanganyikiwa Jamani Inalipa kuwa na YESU Mwenzenu Imelipa kuwa na YESU Jamani Inalipa Kuwa na YESU Oneni Imelipa Kuwa na YESU Mara Mia hapa Mara Mia Kule Haikuwa Hadithi ya Bure Amefidia hata na muda ule Ulioliwa na Madumadu na nzige Wako Wapi Tena Watesi Wangu Wako wale walionidharau Mko Wapi Tena watesi wangu Njooni muonje wema wa Yesu wangu